Kuria East residents smile as Safaricom launches new mast

Safaricom

Safaricom

Na Mwandishi wa Migori News

Wenyeji wa Kegonga eneo bunge la Kuria Mashariki Kaunti ya Migori wamepata afueni baada ya Kampuni ya Safaricom kujenga mnara wa kuimarisha mawasiliano ambayo yalikuwa kizungumkuti katika eneo hilo.

Kwa muda mrefu Mtandao wa Tanzania (Vodacom) na Kenya (Safaricom) imekuwa ikikungamana pamoja na kuifanya mawasiliano ya Kuria Mashariki kuzoroteka.

Kupitia njia ya simu na KNA, naibu wa kaunti komishena wa Kagengo Bwana Kevin Mosambo amesema kwamba, kuimarishwa kwa mawasiliano Kuria Mashariki kumesaidia sana maafisa wa usalama kufanya kazi yao ipasavyo.

“Kwa sasa wanaweza kupiga na kupokea simu kiurahisi na kutoa msaada wa dharura kwa wananchi,” Masombo alisema
Kwa upande mwingine wakazi wa eneo hilo wamejawa na tabasamu kwani shughuli zao za hapa na pale zimerahisishwa kupitia mawasiliano bora.

Mwakilishi wa Wodi ya Nyabasi West Paul Nyangi ambaye Mtandao/Mnara huo ulijengwa kwenye eneo lake (kebaroti) lililo na mwinuko mkubwa, amesema kuwa wananchi wawe makini na viongozi wanao wachagua ili matakwa na mahitaji yao yawe yanatekelezwa kwa muda mfupi.