Kuria East deputy commissioner warns Kuria against circumcising girls

 Some of the rescued girls who escaped FGM at Komotobo Center in Kuria East sub-county


Some of the rescued girls who escaped FGM at Komotobo Center in Kuria East sub-county

Na Mwandishi wa Migori News

Mipango ya Kukeketwa kwa wasichana katika jamii ya WaKuria huenda zisifanyike kama ilivyopangwa na wazee kufuatia serikali kuweka mikakati maalum ya kukabiliana nayo.

Kwenye mkutano uliowashirikisha viongozi na wazee wa kimila Katika Kuria Mashariki, Naibu wa Kaunti Kamishina Bwana Wesley Koech aliwaonya wazee hao vikali na kusema kwamba yuko tayari kumkinga mtoto msichana kutokana na dhuluma zinazomgandamiza katika jamii hiyo.

Bwana Wesley Koech aliwaonya wazee hao vikali na kusema kwamba sheria inamkinga mtoto msichana kutoka kwa dhuluma zinazoweza kuwepukika.

Aliongeza kuwa serikali imemuongezea idadi kubwa ya maafisa wa polisi wa kukabiliana na watakao fanikisha ukeketaji wa wasichana kwa njia moja au nyingine.

Koech alidokeza kwamba wale wanaotaka kuwatahiri watoto wao wa kiume kutipitia mila hizi lazima pia wawe chini ya uwangalizi wa madaktari ili kuepusha maradhi sugu yanayo enea kupitia njia hii na kupunguza pia matumizi ya vifaa hafifu ambavyo huenda vikadhuru afya ya wale wanaopashwa tohara kupitia njia ya kimila.

“Wale wanaopanga kuwapasha tohara wanao wa kiume lazima waende kwa kituo cha afya ili kuepuka maradhi yanayo enea kupitia njia hiyo,” Koech alisema

Kulingana na Afisa wa elimu katika eneo hilo Bwana James Muniko, alisema kwamba iwapo mzazi atapatikana akimfanyia mtoto msichana unyama huu atafungwa jela miaka tano au kutozwa faini kali.

Katika harakati hizo, Mashirika Yasiokua ya Kiserikali yamefungua kambi sehemu mbalimbali Kuria Mashariki ili kumkinga na kumuelemisha mtoto msichana madhara yanayo tokana na ukeketaji huu.