21 livestock dead as famine threatens Bande, Nyatike

Mzoga wa ng'ombe nchini Somali. Picha imenukuliwa mtandaoni

Mzoga wa ng’ombe nchini Somali. Picha imenukuliwa mtandaoni

Na Mwandishi wa Migori News

Wakazi wa eneo la Bande kwenye kaunti ya Migori wanaishi kwa hofu ya kupata ugonjwa wa kipindupindu, homa ya tumbo na kichocho baada ya kiangazi.

Wakazi hao wanaomba serikali ya kaunti ilete mikakati kabambe ya kuzuia janga hilo kwani bwawa la Bande linalotumiwa na wakazi na mifugo linazidi kukauka kufuatia kiangazi hicho.

Wakiongozwa na naibu chifu wa kata ndogo ya Bande Esther Adongo Ochiengi, wakazi hao wanadai kuwa wamepoteza mifugo ishirini na moja.

“Tunatumia anagalau masaa mawili kusaka maji ya kutumia na masaa mingi mno kwa chakula cha mifugo yetu,” Adongo aliiambia shirika hili la habari.

Miongoni mwa wale waliopoteza mifugo yao katika eneo hilo ni mzee Agoro Obinju aliyepoteza mifugo watano, Ochieng Obinju mifugo watatu na Silvance Ogutu mifugo mmoja huku wengine wakikosa kuripoti kufa na kuangamia kwa mifugo wao.

Watatu wao wanasema maeneo yaliyohadhiriwa zaidi ni pamoja na Kanyarwanda, Kadem ya mashariki na Kaler.

“Tunataka serikali ya kaunti na gavana Obado watuambia miradi ya kuleta maji maeneo haya yalifika wapi kwani tunaumia sio haba,” Obinju alisema.